JUMAPILI YA 5 YA PASAKA

Mada ya Jumapili:

Njia kadhaa za kujitoa maisha yako kwa Kristo.
Cha msingi katika masomo ya leo ni uwepo wa “vyumba vingi” kwa nyumba ya Baba wetu, yaani
njia nyingi ambazo tunaweza kuwasaidia wenzetu. Yesu anasema katika Injili ya kwamba, njia ya
kwenda kwa Baba ni kupitia kuwatumikia ndugu na dada zetu. Somo la pili linaashiria jingo
mpya ilhali somo la kwanza inakadiri jinsi wakristo wa karne ya kwanza, wakaazi wa Yerusalemu,
walivyotatua shida iliyowakabili ya ugaavi wa chakula. Masomo yote mawili yanatusaidia
kuelewa ujumbe wa leo.


SOMO LA 1: Matendo 6:1-7.
Siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung’uniko ya
Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika
huduma ya kila siku. Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, “Haipendezi
sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani. Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni
mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya
jambo hili; na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno”. Neno hili likapendeza
machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na
Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;
ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu
yao. Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii
kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.
NENO LA MUNGU.


WIMBO WA KATIKATI: Zaburi. 33:1-2, 4-5, 18-19 (K) 22


(K) Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi, Kama vile tulivyokungoja Wewe. Au: Aleluya
Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
Mshukuruni Bwana kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi wmimbieni sifa (K).


Kwa kuwa neno la Bwana lina adili, Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu. Huzipenda haki na
hukumu, Nchi imejaa fadhili za Bwana. (K)

Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao, Wazingojeao fadhili zake. Yeye huwaponya nafsi zao na
mauti, Na kuwahuisha wakati wa njaa. (K)


SOMO LA 2: 1 Petero. 2:4-9.
Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye
heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani
mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa
kuwa imeandikwa katika maandiko, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni teule,
lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika. Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha. Kwa maana kujikwaza kwa neno
lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo. Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa
kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye
aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.
NENO LA MUNGU.


SHANGILIO:Yohana 14:6.

Aleluya.
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba,
ila kwa njia ya mimi. Aleluya.


INJILI: Yohana. 14: 1-12.


Yesu aliwaambia wafuasi wake: ‘Msifadhaike mioyoni mwenu;
mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba
yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia, maana naenda kuwaandalia mahali.
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi,
nanyi mwepo. Nami niendako mwaijua njia.’ Tomaso akamwambia, ‘Bwana, sisi hatujui
uendako; nasi twaijuaje njia?’ Yesu akamwambia, ‘Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji
kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba, tangu sasa
mnamjua, tena mmemwona.’ Filipo akamwambia, ‘Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.’
Yesu akamwambia, ‘Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo?
Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? Husadiki ya
kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi
siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya
kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! hamsadiki hivyo, sadikini kwa
sababu ya kazi zenyewe. Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo
mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda
kwa Baba.’
INJILI YA BWANA.


SALA WAKATI WA DHIKI KUPITIA KWA MAOMBEZI YA BIKIRA MARIA
WA GUADALUPE.

Ewe Bikira Mtakatifu wa Guadalupe,
Malkia wa Malaika na Mama wa ulimwengu,
Twaukimbilia ulinzi wako leo, sisi wanao wapendwa,
Twakuomba utuombee kwa Mwanao, Yesu,
Ulivyofanya katika harusi ya Kana.
Tuombee, ee Mama mwenye upendo,
Na kuipatia nchi yetu na dunia nzima,
Pamoja na jamii zetu na wapendwa wetu,
Ulinzi wa malaika wako watakatifu,
Ili tuokolewe kutokana na janga hili la virusi vya Korona.
Kwa wote walioathirika,
Twakuomba uwajalie neema ya uponya na ukombozi.
Sikia vilio vya wanyonge na wenye hofu,
Futa machozi yao na uwasaidie kuamini tena.
Wakati huu wa majaribu,
Tufundishe sisi sote tulio Kanisani,
Tupendane, tuwe na subira na wenye ukarimu.
Na utusaidie tulete Amani ya Kristu katika nchi yetu
Na katika nyoyo za watu.
Twaja kwako kwa ujasiri,
Tukijua kwamba wewe kweli ndiwe Mama wetu mwenye huruma,
Afya ya wagonjwa, na chanzo cha furaha yetu.
Tufunike katika vazi lako takatifu la ulinzi,
Tukumbatie mikononi mwako,
Na utusaidie daima tujue upendo wa Mwanao, Yesu. Amina.
Sala Hii imetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na Parokia ya Mama wa Guadalupe – Nairobi, Kenya: kwa
ruhusa ya Kongamano la Maaskofu Wakatoliki wa Marekani.

MATANGAZO YA KANISA
Mei 10. 2020
JUMAPILI YA 5 YA PASAKA


MISA ZA WIKI (Kiingereza)
Katika mtandao
Jumatatu hadi Ijumaa saa moja asubuhi, saa saba na dakika kumi na tano
mchana na saa kumi na moja unusu jioni. Jumamosi saa moja asubuhi
Misa siku ya Jumapili
Jumamosi: Saa kumi na moja unusu jioni
Jumapili: Saa nne asubuhi (Swahili)
na saa sita mchana (Kiingereza)


MATOLEO YA KANISANI
• Fungu la kumi, Sadaka, Church Dues, maombezi maalum, michango ya
kusaidia na kadhalika, tafadhali tumia paybills (zinazowekewa hapa) au
• kwa njia ya bahasha na katika ofisi ya parokia.

PAYBILL / FAMILY BANK LINK.
Select Lipa na M-Pesa Option.
Select PayBill Option
Enter Business Number: 222118
Enter ACCOUNT No: LUPE#
Enter ammount to Give
Enter Your M-Pesa PIN
Press Ok.
Wait For an SMS Notification.


PAYBILL / ECOBANK.
Select Lipa na M-Pesa Option.
Select PayBill Option
Enter Business Number: 698292
Enter ACCOUNT No: YOUR NAME
Enter ammount to Give
Enter Your M-Pesa PIN
Press Ok.
Wait For an SMS Notification.


Giving is Worship
GIVING BACK TO THE ONE WHO FIRST GAVE.

Mothers are the pillars of families and the church and are the back bone of the Economy.Our mother Mary
is the perfect example of a mother who was endowed with love, Patience,Spiritual strength, humbleness and
endurance. Our mothers try to follow her example as the role model.
Mothers make sacrifices for their family without expecting anything in return. They are just happy to see you
happy. They carry you in their heart always. Mothers are special and no one else in this whole universe can
replace the place of a mother in our lives. They do so much for us and never demand for anything in return.
They make us feel special every single day of the year but there is this one day when we can actually make
them feel special and that day is Mother’s Day.
A little show of appreciation goes a long way, and while you can certainly turn Mother’s Day into a big event,
simply hearing from you will make mom smile.
Elina Mutuku
Moderator 2019-2022
Our Lady of Guadalupe parish

Download the full bulletin below


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *